BARUA KWA Babu

*Barua kwa Babu*
Sehemu ya tatu..... yaendelea

Kama kawaida najiliwaza kando ya kaburi la  kio changu msiri wangu Babu.(jua la Zama upepo   mwembamba wavumaa sauti inayo sikika ni nyimbo za makindu utadhani mashindanoni kwa kuimbaa).Babu leo ni  ijuma sijui niende msikitini nijee au tusemezane ndo niende zangu kule kwa *Mulungu*. Roho yangu Ina amani hapa Nina Imani Nita yapata yangu hapa.Leo kwema kuliko Jana afueni ya Leo nayasitiri. Babu  najua  yaleo maswali ni kwako utamaka utashangaa bila Shaka Apo nyuma Leo ningesikia “ *blood hell* ”. Alamisi 31/10/2023 jua likiwa utosini  saa Saba madakika.......pale mwembeni kidogo nitokome kwa dhana kua nimeona malaika. Binti yako wapekee uliye mzawidi kipande Cha ardhi shauku kwakee ndoa ni ndoto za mchana,kajitokezaa kavalia kanzu nyeupe pe! pe! juu Hadi chini nyeupe pe ata sanda tuliyo kufuma  nyeusi kwa kanzu ya *Reverend* .

Duniani Kuna mengi kwa walio hai ishi uyaone. Mkutano wa dharura  ukaketi Hala Hala kila mmoja kanyenyekea  mbele ya malaika.Mjuku wako *Bora Daraja* kinda wangu *kachele  kachila* nyanya kwa unyonge wake kasoro _captain_na  mamangu..chumbani Kimia kimia ata kwa mdaa niliusikia moyo wa kachele ukidundadunda.Habari ya mkutano asijue mtuu *Reverend* mwenye kiti karani na mlinzi mlangoni.

Saa kumi kasoro tik tik tok tok ukutani ndo sauti ilikua yatamba chumbani ukutani picha lako limetukodolea macho kana kwamba wewe ni mwalikwa kwa huu mkutano wa sijui.“ _Basi tuombe”_ sauti ya kuamuru sio swali ndio sauti nilisikia baada ya sali moja...Bila kuchelewa tuliomba dakika kenda... _Nina  habari njema kutoka kwa Baba ( nikagutuka nikashangaa Babu sikuizi  wazungumza na Reverend) wote mmetenda dhambi mama tubuu....weee Bora koma Safari za kaburini.....kachele wapi mamako......kila mmoja alikua na mashtaka tele na onyo Kali...pigo la Mungu babangu ni kifungo Cha nguzo iliyo Baki hili Boma *Captain*...........sote leo tuna tubu na lazima milango ya gereza itafungukaa_.   Kimia kirefu kilitanda.

Wimbo Bora  uliibwa.. _Bwana shuka leo tukuone_ . Maswali kwangu mengi Mimi mwenyewe mjuku wa Daraja ndatubu kivipii ndaanzaje nimwambie Nini *Mulungu*. maombii ya kufufua mtuu yaliombwaa kwa mdaa wa lisaa moja bila kupumua wala kushusha sauti malaika kaomba kweli ataa kwa mdaa Imani ilinipanda kidogo nitoe picha yako ukutani  nilijihisi msaliti.....Mara ya kwanza nyanya kasimama wima......ya mungu hayo usiniulize kivipi. Baada ya maombii tukaketi kungoja matokeo ya Liotarajiwa alivyo sema mwenyewe “anytime from now ”. Langu jicho kachele kamaliza ndoto ya kwanza nyanya kasinzia.

Saa moja jioni dakika hamsini kwenye saa ya ukuta.Nilikua macho sio ndotoni *.Saha kahawa Daraja*, captain aliubisha mlangoo..................


@prof. George Daniel Meya.

Comments

Popular posts from this blog

PAINFUL BLESSINGS

she broke it

MY ROYAL HOME