BARUA KWA BABU

*BARUA KWA BABU* 

 _SEHEMU YA SITA._ 

Safari ya panda shuka Milima mabonde lala amka mwishowe ilitufikisha *kokotoni* baada ya kusafiri usiku kuchaa. Safarini mazungumzo yangu na baba yalikuwa machache sana Mara kwa Mara ilikuwa swali jibu lakini wakati mwingine wote kila mtu alijiwaza yalio mhusu Maishani mwake.Baba alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo macho yetu yaligongana mdaa baada ya mdaa na wakati huu wote Nilimwona akijinong'onezea vijimambo.kwa hakika mama alikua ubavu wa baba,tangia habari za kutoweka kwa mama baba alikua mnyonye na mtu na moyo wake Mara ya mwisho kumwona Baba hivi ni wakati wa kifo Cha babake Rafiki yangu Babu.

Jua la utosini liliangaza bila huruma kanakwamba kule juu  kunaye aliyelichochea kuni lizidi kushika kasi afueni upepo ulio kuwa wavuma vuma. *HAPA  NI KOKOTONI CHUNGA.* Kibanda kimoja si chambele si chanyuma kizee kizee kimezibwa utakuta pande moja na makindu kilikua na  bango la maandishi haya maandiko mazee hata wino karibu wote umefuta..Nina mgeni asijue aendapo? Nichunge Nini? Kwa Nini mwandishi aliweka hadharani maandishi haya.Nilibaki na maswali kwangu mengi kwa  ilani hiyo makaribisho hayo tarifa hiyo au niseme onyo hiyo. Ajuaye Siri ya kaburi ni marehemu.

 _KOKOTONI CHUNGA_ Kijiji na nusu kina sifa za shetani la sifa za Yesu. Kijiji mazingira yake yalivutia Sana yalipambwa na Minazi mirefu mirefu  upepo mwembamba wa baharini ulivuma vuma na kuzindisha sifa zake. Wakokoto ni watu na *Mila* tamaduni. Nilijikuta kwa kumbukumbu ya maisha ya Babu hadithi zake tukiwa malishoni hapo ndipo niliukumbuka  msemo wake *ukitaka jiko tembea kokotoni.*  Sikuelewa manenoo yake lakini Leo baada ya miaka mitano Rafiki Babu nilimwelewa. Wamama kwa wasichana wote walivalia mavazi  marefu mepesi yenye maua maua kule kwetu tuliyaita *Dera Dera*  akina baba na wavulana walivalia kapturaa wengi miguni kavalia *gurudumu gari* kwa jina  tulilo Vita hivyo viatu kadhu ndefu ndefu ilifanya Kijiji kizima kionekana Kama shule utadhani ni sare kuu ya wakokotoni.

Mtu ni chakula, tulisimama mkahawani moja banda moja sawa sawa na lile la maandishi kukukuu.Karibuni wageni kijize kimoja Babu kilitukaribisha kwa furaha na wema _karembo letea wageni maji.._ msichana mmoja mwembamba umri wangu umbo lake la chupa uso unao ng'ara ng'ara maji kunde kipuli puani  mrefu wa kimo alileta maji glasi mbili. Haikuchukua mdaa kuona vishimo shimo shavuni mwa *karembo* kwa kweli nasadiki Babu ukitaka *jiko* muulize babangu kokotoni ni wapi. Jina mtu *karembo* alipendeza umbo lake mwendo wake wa sitaki nataka  alitembea hima hima uku kutoka juu Hadi chini narekodi kichwani mwangu.  Karibuni wageni sauti nzuri ya kudekeza ilifanya nimkumbuke mamangu kokotoni Kuna Barak na warembo Kama si *karembo* . Sima kwa papa ilitosha shibe zetu. Aki Babu yangu *Daraja* marehemu  nitamwoa mkokotoni.

Muda wa saa nzima pale kwa karembo niliyasikia mengi na kwelewa kwa Nini kile kibango ni ilani.alisema mengi yakale ya kisasa na ata yajayo. _Hapa kokotoni hatuchezewi kusini kaskazini kushoto kulia wote uvuli wao ni hapa Cha mkokotoni hakipotei_ _Wala kuibiwa  hapa kwetu dawa ni sisi_ . Kwa kweli kokotoni kulikuwa na sifa kwote *washirikina* kupindukia wasiri wa dunia la giza watundu wa *elimu* . Wasomi  walihesabika kwa viganja  shida na taaabu ya utamaduni elimu ni Mambo mengineo kwa wakokotoni wazee kwa vijana walibugia pombe marufu kwa jina *mnazi dawa* pombe kileo kiliyo kamuliwa na kutoka kwa mnazi kila Boma kokotoni halikosi *Mgema* ..... _nyumba si mlango._ Yapo mengi mazuri kokotoni vile vile yapo maudhi kakotoni... 

 *Welcome home* mwendo wa saa tisa Robo Babu alitukaribisha kwa hekalu lake..........

@, Prof George Daniel Meya

Comments

Popular posts from this blog

PAINFUL BLESSINGS

she broke it

MY ROYAL HOME