BARUA KWA BABU

*Barua kwa Babu*

Shikamo Rafiki,Nina *one two* nataka niseme nawe ni mdaa nimekua kimia vya kutoshaa... kwanza habari za Bibi Ninazo Tangu utwache amebaki si wa leo si wa kesho uliondokaa na furaha yake.
Mwanao mkubwa babangu tangu uondoke anajulikana Kama  “ *captain* " anabugia pombe kupita kiasi utadhani babake kambariki na mrijaa wa pombe...... Babu ivi Leo ungeli gutukaa tu...ungali duwaa kwa Mambo yanavyo badilika kwa kasi.....Nani Leo angalia jua   binti yako cheupee angalitwaa “ *Reverent* ” cheupe ni mshikadini kupindukia siku hizi inasemakana yeye na Mungu wanachatiii......

Babu nakumbuka vizuri ulinisema nipitapo makaburini niwe kinda kinda kwa kua mizimu siku zote ziko machoo....Basi Leo Niko apa kaburini Nina yangu ya kukulongea... Rafiki wakumbuka ile ndoto yangu ya kua Rubani uliipenda na tuliijivunia maono hayoo Ila babu Nina ati ati Leo juzi badala niote nikiwa napeperushaa ndege ( *Air force one)* niliotaa ninagemaa ......Babu Mimi Rubani nafanya nini juu ya mnazii na kopo la mgema.. nasikitika moyoni Natamani ungekua hai ungenisaidie kwa wakati huu mgumu................Nina mengi Babu lakini tutaonana paradiso tusemezane........

@prof Daniel George Meya

Comments

Popular posts from this blog

PAINFUL BLESSINGS

she broke it

MY ROYAL HOME